Utabiri sahihi zaidi na kamili wa hali ya hewa! Meteored hukupa taarifa ya kina kuhusu hali ya hewa kwa siku 14 zijazo, hali ya hewa ya sasa, tahadhari za hali ya hewa, rada ya mvua, halijoto, ubora wa hewa, viwango vya chavua, unyevu na mambo mengine mengi. Kiolesura chetu ambacho ni rahisi kutumia na kinachoweza kubinafsishwa kimerahisisha njia ya kuangalia hali ya hewa katika wakati halisi, kuliko hapo awali.
Jua jinsi inavyoweza kukusaidia kujua hali ya hewa kwa urahisi zaidi!
KWA NINI UNAPASWA KUPAKUA PROGRAMU YETU?
Kinachotufanya tuwe tofauti ni uwezo wetu wa kutabiri hali ya hewa katika eneo lako mahususi. Huwa tunatumia teknolojia ya kisasa ili kukusanya data, na timu yetu ya wanametolojia huchanganua data hiyo ili kukupa utabiri sahihi na wa kisasa. Tuna uzoefu wa zaidi ya miaka 20 wa utabiri wa hali ya hewa.
Ukibiringiza chini kwenye kiolesura chetu, utagundua:
RADA YA MVUA, RAMANI NA SATALAITI
Ukiwa na rada yetu ya hali ya juu ya mvua, utaweza kufuatilia utabiri wa mvua kwa kutumia data ya uchunguzi kwa usahihi wa uhakika. Kitazamaji chetu cha ramani ya hali ya hewa kina matabaka kadhaa ya utabiri kama vile halijoto, mvua, theluji, kanieneo ya angahewa... na yote yana chembechembe zilizohuishwa zitakazokusaidia kuona mwelekeo wa upepo na mawimbi. Pia tuna picha za satalaiti kuanzia saa 12 zilizopita.
TAHADHARI RASMI NA MAONYO
Usijali kuhusu hali mbaya zaidi za hali ya hewa, kwa sababu tunatoa tahadhari za Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Kenya na za watoa huduma wengine rasmi wa tahadhari za hali ya hewa duniani kote. Utapokea arifa za tahadhari kutoka kwa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Kenya. Tutaendelea kukujulisha kuhusu hali mbaya za hewa katika eneo lako.
UBORA WA HEWA NA MIZIO
Kuna taarifa ya kina kuhusu ubora wa hewa, unyevu, upepo na hali nyingine husika za kuzingatia kwa ajili ya mizio ambayo huenda ikakuathiri. Hii itakusaidia kufanya maamuzi kuhusu shughuli zako za nje na kulinda afya yako.
MACHEO NA MACHWEO NA AWAMU ZA MWEZI
Tunapenda mazingira ya asili, kwa hivyo huwa tunatoa taarifa na michoro kuhusu falaki kama vile macheo na machweo, saa za mchana zilizosalia na awamu za mwezi ili uweze kupanga wakati wa kutembelea, kuendesha baiskeli au shughuli za uvuvi.
HABARI ZA HALI YA HEWA, MAMBO YA KUVUTIA NA SAYANSI
Isitoshe, huwa tunachapisha habari na makala za hali ya hewa zinazofaa na za kisasa kuhusu matukio muhimu ya hali ya hewa. Timu yetu ya wataalamu na wahariri wa kitaifa na kimataifa watakujulisha kuhusu habari za hivi punde na mabadiliko ya utabiri, ili uweze kupanga shughuli zako.
KIOLESURA KINACHOFAA KILA MTU
Kila kizazi kinaweza kukitumia kwa urahisi na hubadilika kulingana na vifaa vyako vyote. Iwe wewe ni mpenda hali ya hewa au unataka tu njia ya haraka ya kujua hali ya hewa, utafurahia kiolesura chetu ambacho ni rahisi kutumia na kinachoweza kubinafsishwa, kilicho mandhari ya rangi na vipimo vinavyokufaa zaidi.
WIJETI
Tuna wijeti zinazokuruhusu uone utabiri wa hali ya hewa moja kwa moja kwenye skrini yako ya nyumbani. Unaweza kuweka wijeti za ukubwa tofauti zenye taarifa husika kama vile halijoto ya sasa, mvua na zaidi. Unaweza kutazama hali ya hewa kwa urahisi bila kulazimika kufungua programu.
HALI YA HEWA KWENYE KIFUNDO CHA MKONO WAKO
Ikiwa una Apple Watch, unaweza kuwa na programu yetu kwenye mkono wako. Unaweza kuangalia ikiwa mvua itanyesha mahali ulipo au hata kuongeza vipengele kwenye saa yako.
DATA YA ULIMWENGU
Pata utabiri unaofaa zaidi wa eneo lako la sasa au utafute maeneo unayopenda kutoka kwa maeneo zaidi ya 6,000,000 kote ulimwenguni. Inapatikana katika zaidi ya nchi 50 na lugha 20.
Kwa kutumia programu hii, unakubali sera ya faragha, sheria na masharti ya Meteored.
Ilisasishwa tarehe
23 Mac 2025