Nukuu Papo Hapo na Arifa

3.8
Maoni elfu 190
1B+
Vipakuliwa
Daraja la maudhui
Kila mtu
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini
Picha ya skrini

Kuhusu programu hii

Programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti huwawezesha viziwi na watu wenye matatizo ya kusikia kufikia mazungumzo ya kila siku na sauti zinazowazingira kwa urahisi zaidi, ukitumia tu simu yako ya Android.

Kwenye vifaa vingi, unaweza kufungua programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti kwa kufuata hatua hizi:
1. Fungua programu ya Mipangilio kwenye kifaa chako.
2. Gusa Ufikivu
3. Kulingana na kipengele ambacho ungependa kutumia, gusa Nukuu Papo Hapo au Arifa kuhusu Sauti

Unaweza pia kutumia kitufe cha zana za ufikivu, mguso au Mipangilio ya Haraka ili kufungua programu ya Nukuu Papo Hapo au kipengele cha Arifa kuhusu Sauti (https://g.co/a11y/shortcutsFAQ).

Manukuu katika muda halisi
• Pata manukuu katika muda halisi kwa zaidi ya lugha na lahaja 120. Weka maneno maalum unayotumia mara kwa mara, kama vile majina au bidhaa za nyumbani.
• Weka simu yako katika hali ya kutetema mtu anapotamka jina lako.
• Andika majibu katika mazungumzo yako.
• Tumia maikrofoni za nje zinazopatikana katika vifaa vya sauti vyenye waya, vifaa vya sauti vya Bluetooth na maikrofoni za USB ili kupokea sauti vizuri zaidi.
• Kwenye simu zinazokunjika, onyesha manukuu na majibu yaliyoandikwa kwenye skrini ya nje ili iwe rahisi kuwasiliana na wengine.
• Chagua kuhifadhi manukuu kwa siku 3. Manukuu yaliyohifadhiwa yatasalia kwenye kifaa chako kwa siku 3 ili uweze kuyanakili na kuyabandika kwingineko. Kwa chaguomsingi, manukuu hayahifadhiwi.

Arifa kuhusu Sauti
• Pata arifa kuhusu sauti muhimu karibu nawe, kama vile king'ora cha moshi kinapolia au mtoto anapolia.
• Weka sauti maalum ili upate arifa vifaa vyako vinapolia.
• Kagua sauti kutoka saa 12 zilizopita ili usikie kilichofanyika karibu nawe.

Mahitaji:
• Android 12 na matoleo mapya zaidi

Programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti imeundwa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Gallaudet, chuo kikuu cha Viziwi na watu wenye matatizo ya kusikia kinachoongoza nchini Marekani.

Usaidizi na maoni
• Ili kutoa maoni na kupata taarifa kuhusu bidhaa, jiunge na Kikundi kwenye Google cha Ufikivu kupitia https://g.co/a11y/forum
• Ili kupata usaidizi wa kutumia Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti, wasiliana nasi kupitia https://g.co/disabilitysupport

Ilani ya ruhusa
Maikrofoni: Programu ya Nukuu Papo Hapo na Arifa kuhusu Sauti inahitaji kufikia maikrofoni ili kunukuu matamshi na sauti zilizo karibu nawe. Sauti haihifadhiwi baada ya manukuu au sauti zilizotambuliwa kuchakatwa.
Arifa: Vipengele vya Arifa kuhusu Sauti vinahitaji uwezo wa kufikia arifa ili kukuarifu kuhusu sauti.
Vifaa vilivyo karibu: Programu ya Nukuu Papo Hapo inahitaji uwezo wa kufikia vifaa vilivyo karibu ili kuunganishwa na maikrofoni zako za Bluetooth.
Ilisasishwa tarehe
31 Mac 2025

Usalama wa data

Usalama huanza kwa kuelewa jinsi wasanidi programu wanavyokusanya na kushiriki data yako. Faragha ya data na mbinu za usalama zinaweza kutofautiana kulingana na matumizi yako, eneo ulilopo na umri wako. Msanidi programu ametoa maelezo haya na anaweza kuyasasisha kadiri muda unavyopita.
Hakuna data inayoshirikiwa na wengine
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wasanidi programu wanavyobainisha kushiriki data
Programu hii huenda ikakusanya aina hizi za data
Taarifa binafsi, Sauti na nyingine3
Data inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa
Data haiwezi kufutwa
Ukaguzi huru wa usalama

Ukadiriaji na maoni

3.8
Maoni elfu 185

Vipengele vipya

• Uwezo wa kutumia Dual Screen kwenye simu zinazokunjika. Hali za utumiaji zinaweza kutofautiana kulingana na simu.
• Uwezo wa kutumia lugha zaidi nje ya mtandao, zikiwemo Kihindi, Kikorea, Kipolandi, Kireno, Kirusi, Kichina Kilichorahisishwa, Kichina cha Jadi, Kituruki na Kivietnamu.